Kwenye Mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) uliofunguliwa rasmi Oktoba 16 hapa Beijing, Xi Jinping alitoa hotuba kwa niaba ya Kamati Kuu ya 19 ya CPC. Kwenye hotuba yake, Xi ameweka mpango wa kimkakati kuhusu kuijenga China kuwa nchi ya kisasa ya kijamaa kwa pande zote, na kufafanua umaalum muhimu na matakwa ya kimsingi ya ujenzi huo, hotuba ambayo imefuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa.
Mkuu wa Taasisi ya Sera za Afrika yenye makao yake makuu mjini Nairobi, Profesa Peter Kagwanja, amepongeza mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC unaoendelea hapa mjini Beijing. Kagwanja amesema hotuba ya Rais Xi Jinping ya ufunguzi wa mkutano huo Jumapili imegusia maswala muhimu kwa China na dunia kama vile kushiriki kwenye uongozi wa kimataifa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC ulianza jana mjini Beijing, huku viongozi wa vyama vya kisiasa vya nchi mbalimbali za Afrika wakitoa salamu za kupongeza kufanyika kwa mkutano huo, kwa kamati kuu ya CPC na kwa katibu mkuu wake Xi Jinping. Mwenyekiti wa chama cha ANC cha Afrika Kusini ambaye pia ni Rais wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa, amesema mkutano mkuu wa 20 wa CPC unafanyika wakati hali ya dunia inashuhudia mabadiliko makubwa.
Oktoba 16, Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ulifunguliwa katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.