Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC umechagua Kamati Kuu mpya na Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu mpya kabla ya kufungwa leo Jumamosi.
Xi Jinping ameendesha kikao cha ufungaji cha Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China uliofanyika leo Jumamosi kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.
Mkutano Mkuu wa 20 wa chama tawala cha China Chama cha Kikomunisti cha China CPC uliofanyika kwa siku 7 umefungwa leo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing. Mkutano huo umechagua Kamati Kuu ya 20 ya CPC na Kamati Kuu ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhamu, kupitisha azimio kuhusu ripoti ya kazi ya Kamati Kuu ya 19 ya CPC, kupitisha azimio kuhusu ripoti ya kazi ya Kamati Kuu ya 19 ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC, na azimio kuhusu marekebisho ya katiba ya CPC.
Kituo cha waandishi wa habari cha Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kimeandaa mkutano na waandishi wa habari uliopewa mada isemayo "Chini ya Mwongozo wa Fikra ya Xi Jinping juu ya Diplomasia, Kusonga Mbele na Kujitahidi Kujenga Msingi Mpya wa Diplomasia ya nchi kubwa yenye Umaalumu wa China" hapa Beijing, China, Oktoba 20, 2022. Shen Beili, Naibu Mkuu wa Ofisi ya Mambo ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya CPC, na Ma Zhaoxu, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, walihudhuria mkutano huo na waandishi wa habari.