Ma Zhaoxu, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing, China, Oktoba 20, 2022. Kituo cha waandishi wa habari cha Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) siku ya Alhamisi kiliandaa mkutano wa waandishi wa habari wenye mada isemayo "Chini ya Mwongozo wa Fikra za Xi Jinping juu ya Diplomasia, Kusonga Mbele na Kujitahidi Kujenga Msingi Mpya wa Diplomasia ya nchi kubwa yenye Umaalumu wa China".
BEIJING - Kwa wengi, mmea wa moss si chochote ila mmea mdogo mdogo unaokua katika sehemu zisizo na thamani zenye unyevunyevu, lakini kwa wanakijiji katika mji mdogo wa milimani wa Maoyang nchini China, mmea huu umeleta pesa na kuwaondoa kwenye umaskini na kuwaweka kwenye safari ya kupata utajiri zaidi. Mji huo wa mbali uko katika tarafa moja kati ya tarafa zenye maendeleo duni zaidi katika Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, mkoa wenye nguvu kubwa kiuchumi na wa majaribio katika kufikia ustawi wa pamoja wa watu wote wa China.
Kituo cha wanahabari cha Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha CPC kimeandaa mahojiano yake ya kundi la nne Jumatano wiki hii. Kwenye mahojiano hayo, wasemaji waliufahamisha umma na waandishi wa habari kuhusu uelewa wao na majadiliano ya wajumbe kuhusu ripoti ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC, na kujibu maswali kutoka kwa wanahabari.
BEIJING – Mchakato wa maendeleo ya mambo ya kisasa ya China, ambao ni eneo muhimu linalofafanua safari ya China ya ustawishaji mpya wa taifa, kwa mara ya kwanza umeandikwa katika ripoti ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), chama kikubwa cha Ki-Umarxi kinachoongoza duniani. Katika ripoti yake ya Jumapili kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China, Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, alisisitiza "kazi kuu" ya Chama, akitaka juhudi za ustawishaji wa Taifa la China katika sekta zote "kupitia njia ya China ya maendeleo ya mambo ya kisasa.