Beijing. Wakati kukiwa na ukosoaji mwingi duniani kuhusu sera ya China ya kupambana na ugonjwa wa Uviko-19 maarufu ‘zero covid policy’, Chama tawala nchini humo kimeitetea kikisema imekuwa msaada mkubwa kwa nchi.
---Wataalamu wa kigeni watafsiri watoa maoni juu ya Ripoti ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha CPC Wataalamu tisa wa kigeni wa lugha nane za Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kiarabu, Kijerumani, Kijapan na Kilaos walikuwa wamealikwa kushiriki kwenye tafsiri za lugha mbalimbali za Ripoti ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China. Wataalamu hao ni watu waliopata mapema zaidi nakala za ripoti hiyo.
Oktoba 17, Xi Jinping alishiriki kwenye majadiliano ya wajumbe wa Mkoa wa Guangxi wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China(CPC). (Mpiga picha: Xie Huanchi/Xinhua).
Zhao Chenxin, Naibu Mkurugenzi wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya Taifa akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari katika Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC ambao unaendeleo hivi sasa hapa Beijing, China Oktoba 17, 2022. (Xinhua/Zhang Yuwei) Naibu Mkurugenzi wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya Taifa ya China Zhao Chenxin Jumatatu ya wiki hii alisema, China itashikilia kithabiti kupanua ufunguaji wa mlango kwa pande zote, kuhimiza utandawazi wa uchumi wa dunia uendelee kwa mwelekeo wa uwazi zaidi, shirikishi zaidi, uwiano zaidi na kupata maendeleo kwa pamoja.