BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amerejea Beijing Alhamisi usiku baada ya kuhudhuria Mkutano wa 16 wa Viongozi wa Nchi za BRICS uliofanyika Kazan, Russia kuanzia Oktoba 22 hadi 24. Msafara wa Rais Xi, ambao ni pamoja Cai Qi, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati Kuu ya CPC, na Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China, umerejea kwa ndege moja.
Rais wa Russia Putin akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari katika siku ya mwisho ya Mkutano wa 16 wa Viongozi wa Nchi za BRICS mjini Kazan, Russia Oktoba 24. (Xinhua/Cao Yang) MOSCOW - Nchi za BRICS zina dhamira ya kujenga utaratibu wa dunia wa kidemokrasia na wenye pande nyingi, Rais wa Russia Vladimir Putin amesema siku ya Alhamisi, kwenye mkutano na waandishi wa habari katika siku ya mwisho ya Mkutano wa 16 wa Viongozi wa Nchi za BRICS mjini Kazan, Russia.
Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba muhimu yenye kichwa "Kuunganisha Nguvu Kubwa ya Nchi za Kusini Kujenga Pamoja Jumuiya ya Binadamu yenye Mustakabali wa Pamoja" kwenye mazungumzo ya viongozi wa nchi za "BRICS Plus" huko Kazan, Russia, Oktoba 24, 2024. (Xinhua/Li Xueren) KAZAN, Russia - Wakati viongozi wa nchi za BRICS walipokutana na nchi zisizo wanachama zinazotafuta uhusiano wa karibu na jumuiya hiyo siku ya Alhamisi, Rais wa China Xi Jinping ameeleza uungaji mkono mkubwa kwa Nchi za Kusini wakati akishiriki kwenye mazungumzo ya viongozi wa nchi za "BRICS Plus" siku ya mwisho ya mkutano huo wa Kazan.
Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba muhimu yenye kichwa "Kuunganisha Nguvu Kubwa ya Nchi za Kusini Kujenga Pamoja Jumuiya ya Binadamu yenye Mustakabali wa Pamoja" kwenye mazungumzo ya viongozi wa nchi za "BRICS Plus" huko Kazan, Russia, Oktoba 24, 2024. (Xinhua/Li Xueren) KAZAN, Russia - Rais Xi Jinping wa China jana Alhamisi alipokuwa akihutubia katika mazungumzo ya viongozi wa "BRICS Plus" ametoa wito kwa nchi za "BRICS Plus" kujitahidi kwa ajili ya usalama wa pamoja, maendeleo ya pamoja na mapatano kati ya ustaarabu mbalimbali.