人民网首页

Habari

China na Tanzania zakubaliana kutekeleza kwa pamoja mikakati ya maendeleo

(Picha inatoka tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China.) Tanzania na China zimetoa taarifa ya pamoja zikiahidi kutekeleza kwa pamoja mikakati ya maendeleo ili kuboresha maendeleo ya pamoja.

China na Afrika Kusini zatoa wito wa ushirikiano wa karibu kati ya Kusini na Kusini

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ambaye kwa sasa yupo ziarani katika nchi za Afrika, alifanya mazungumzo kwa njia ya simu Jumamosi na mwenzake wa Afrika Kusini, Ronald Lamola, akitoa wito kwa nchi zote mbili kuunga mkono mifumo ya pande nyingi na kuimarisha ushirikiano kati ya Kusini na Kusini. Wang, amekipongeza chama tawala cha Afrika Kusini, African National Congress (ANC) kwa maadhimisho ya miaka 114 tangu kuanzishwa kwake, akielezea imani kwamba kupitia juhudi za pamoja za ANC, Afrika Kusini itaungana kukabiliana usumbufu kutoka nje na kufikia maendeleo na ustawi wa kitaifa.

China na Lesotho zaapa kusukuma mbele ushirikiano wa kimkakati hadi ngazi ya juu zaidi

(Picha inatoka tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China.) Lesotho na China zimethibitisha tena dhamira yao ya kusukuma mbele ushirikiano wa kimkakati wa pande mbili hadi ngazi ya juu na kuufanya kuwa mfano wa mawasiliano ya kirafiki na maendeleo ya pamoja kati ya nchi zenye hali na mifumo tofauti ya kitaifa.

Kuadhimisha miaka 70 ya uhusiano wa kidiplomasia, China na Afrika zaimarisha ushirikiano katika kusukuma mbele mambo ya kisasa

Hafla ya uzinduzi wa Mwaka wa 2026 wa Mawasiliano kati ya Watu wa China na Afrika ikifanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Januari 8, 2026. (Xinhua/Han Xu) JOHANNESBURG - Mwaka huu unatimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Afrika.

Iliyopita7 8 9 10 11 Inayofuata