Wanafunzi wa Tanzania wakijifunza kupika baozi kwa mvuke huko Dar es Salaam, Tanzania, Januari 28, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman) DAR ES SALAAM – Ndani ya jiko lenye pilikapilika nyingi katikati ya jiji la Dar es Salaam, Ruth Washima Seni, mwanafunzi kijana wa mambo ya hoteli nchini Tanzania, anajaribu kukata viazi mviringo katika vipande vyembamba kama nywele.
Picha hii ya kumbukumbu isiyo na tarehe ikionyesha mandhari ya Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Nishati ya Upepo cha Aysha II katika Jimbo la Somali, Ethiopia. (Kampuni ya Umeme ya Dongfang/kupitia Xinhua) ADDIS ABABA - Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Jumamosi alizindua mradi wa kipindi cha kwanza wa Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Nishati ya Upepo cha Aysha II katika Jimbo la Somali, akisisitiza kwamba maendeleo ya nishati safi ni kiini cha kazi ya muda mrefu ya kubadilisha mundo wa uchumi wa nchi hiyo.
Kenya inaongeza juhudi ili kuendeleza sekta yake ya filamu kwa kutafuta uwekezaji na ushirikiano na wawekezaji wa China. Mwenyekiti wa Kamisheni ya Filamu ya Kenya Bw.
Matumizi ya nishati ya kijani barani Afrika yameongezeka kwa kasi kutokana na upatikanaji wa suluhisho la bidhaa za ubora wa juu na gharama nafuu za umeme wa jua zinazotengenezwa nchini China. Meneja wa mradi katika Kituo cha Uwezo wa Nishati, Mazingira na Uchumi Endelevu katika Kampuni ya Huduma ya AHK East Africa, Georg Pflomm amesema, bidhaa zinazotumia nishati ya jua zinazotengenezwa nchini China zimeboresha upatikanaji wa nishati na usalama katika bara la Afrika linalotaka kuendeleza utoaji mdogo wa hewa ya kaboni.