Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Mahmoud Ali Youssouf wakifanya kwa pamoja Mazungumzo ya tisa ya Kimkakati kati ya China na AU kwenye makao makuu ya AU mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Januari 8, 2026. (Xinhua/Han Xu) Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Mahmoud Ali Youssouf kwa pamoja wamefanya Mazungumzo ya 9 ya Kimkakati kati ya China na AU kwenye makao makuu ya Umoja huo mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi jana Alhamisi alikutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Gedion Timothewos mjini Addis Ababa, huku pande hizo mbili zikiahidi kusukuma mbele kwa pamoja utekelezaji wa matokeo yaliyopatikana kwenye Mkutano wa Kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa kwa wanahabari, pande hizo mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja zote na kujitahidi kujenga uhusiano wa kimkakati wa hali zote kati ya China na Ethiopia kuwa mfano wa kuigiwa kwa ajili ya kujenga Jumuiya ya hali zote ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mapya.