Ubalozi wa China nchini Sudan Kusini umetoa msaada wa zaidi ya vifaa 20 vya mashine za kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula katika mkoa wa Ikweta Magharibi nchini humo. Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo hapo jana, msaidizi wa katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi wa Amani Pia Philip Michael amesema, vifaa hivyo vitaboresha usalama wa chakula na kusaidia juhudi za ujenzi wa amani katika mkoa huo ambao umeshuhudia mapigano ya kikabila tangu mwaka 2021.
Mjumbe Maalum wa Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Umma la China Bw. Zheng Jianbang amehudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais mpya wa Guinea, Mamady Doumbouya iliyofanyika Conakry, mji mkuu wa nchi hiyo juzi Jumamosi na kufanya mazungumzo naye.
Ubalozi wa China nchini Afrika Kusini jana Jumatatu mjini Pretoria ulifanya hafla ya kusherehekea uzinduzi wa Mwaka 2026 wa Mawasiliano kati ya Watu wa China na Afrika. Mwaka huu pia ni maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na nchi za Afrika.
BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema jana Jumatatu kwamba kanuni ya kuwepo kwa China moja ni makubaliano ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa na kanuni ya msingi inayosimamia uhusiano wa kimataifa, pia ni msingi wa kisiasa wa uhusiano kati ya China na Afrika. Mao Ning ameyasema hayo kwenye mkutano wa kawaida na waandishi wa habari alipoulizwa kutoa maoni kuhusu kauli za mamlaka za Taiwan juu ya kanuni ya kuwepo kwa China Moja, kama ilivyoelezwa kwenye taarifa ya pamoja ya Mazungumzo ya 9 ya Kimkakati kati ya China na Umoja wa Afrika (AU).