Ethiopia itafunga ofisi yake ya ubalozi nchini Misri kwa muda kuanzia Mwezi Oktoba

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 28, 2021

Habari zilizotolewa tarehe 26 kwenye tovuti ya piramidi ya kiserikali ya Misri zilisema kuwa, siku hiyo balozi wa Ethiopia nchini Misri, Bw. Markos Tekle Rike alisema, kutokana na sababu ya fedha, ofisi ya ubalozi wa Ethiopia nchini Misri itafungwa kwa miezi mitatu hadi sita kuanzia Mwezi Oktoba.

Siku hiyo Bw. Rike alisema channel ya Kiarabu ya Kampuni ya utangazaji ya Uingereza BBC kwamba, kufungwa kwa ofisi ya ubalozi nchini Misri ni kwa ajili ya kupunguza matumizi ya fedha, uamuzi huu hauhusiani na swala la “Boma la Grand Rianissance la Ethiopia” kati ya Ethiopia, Misri na Sudan.

Habari zilisema kwamba, kutokana na sababu ya kiuchumi, Ethiopia imeamua kufunga kwa muda ofisi zake za ubalozi katika nchi zaidi ya 30, zikiwemo Canada na nchi nyingine ya za ghuba.

“Bwawa la Mto Nile (GERD)” liko kwenye Mto Nile ya Buluu ambalo ni moja ya vyanzo vikuu viwili vya Mto Nile, bwawa hilo linakaribia mpaka kati ya Ethiopia na Sudan. Serikali ya Ethiopia iliweka jiwe la msingi kwa “Bwawa la Mto Nile (GERD)” mwaka 2011, na ilitangaza kukamilisha kazi ya kipindi cha kwanza cha kuhifadhi maji Mwezi Julai, mwaka 2020. Baadaye, serikali ya Ethiopia ilisema, itaanzisha kipindi cha pili cha kuhifadhi maji, lakini kwa kuwa Misri na Sudan zina wasiwasi kuwa hii itaathiri matumizi salama ya maji ya nchi zao, ambazo ziko sehemu ya chini ya Mto Nile, mazungumzo ya pande tatu yamekwama sasa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha