Ndege ya kivita ya Russia yaambatana na ndege ya upelelezi ya Marekani kuruka kwenye anga juu ya Bahari Nyeusi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 30, 2021

Tarehe 28, makao makuu ya ulinzi wa taifa wa wizara ya ulinzi ya taifa ya Russia yalitoa taarifa yakisema kwamba, ndege moja ya kivita ya Russia-27 ya eneo la kijeshi la kusini la Russia siku hiyo iliambatana na ndege moja ya upelelezi ya Marekani illiyokaribia mpaka wa anga ya Russia katika urukaji wake kwenye anga juu ya Bahari Nyeusi

Taarifa ilisema, mapema ya siku hiyo, rada ya Russia iligundua kitu kimoja kwenye anga juu ya Bahari Nyeusi, ambacho kilikuwa kinakaribia mpaka wa Russia. Halafu ndege moja ya kivita ya Russia-27 ya eneo la kijeshi la kusini iliruka angani, kutambua kitu hiki ni

nini, ili kukizuia kisivamie mpaka. Kupitia kuthibitisha, kitu kicho kilichoko angani ni ndege ya upelelezi ya kimkakati ya Marekani RC-135, ndege ya kivita ya Russia iliambatana nayo katika urukaji wake kwenye anga juu ya Bahari Nyeusi.

Taarifa ilisema kwamba, katika muda wote wa urukaji, ndege ya kivita ya Russia ilikuwa inafuata kwa umakini kanuni za matumizi ya eneo la anga la kimataifa. Baada ya ndege ya upelelezi ya Marekani kuondoka kutoka mpaka wa Russia, ndege ya kivita ya Russia ilirudi salama kwenye kituo chake.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha