Ufunguzi wa COP 15 wafika na jumba lake liko tayari kuwakaribisha wageni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 11, 2021
Ufunguzi wa COP 15 wafika na jumba lake liko tayari kuwakaribisha wageni

Kuanzia tarehe 11 hadi 15, Oktoba, Mkutano wa 15 wa pande zilizosaini “Mkataba wa Anuwai ya Viumbe”wa Umoja wa Mataifa UN (COP 15) utafunguliwa huko Kunming, China, ambao unaitwa “mji wa Spring”.

Kwenye ukumbi wa jumba wa kufanyia mkutano huo, mwandishi wa habari ameona kuwa, maandalizi ya mkutano yamekamilika, kila kitu kiko tayari, na mapambo ya usanifu mzuri kuhusu uhifadhi wa anuwai ya viumbe yanaonekana kila kona. Hali ya shamrashamra ya kukaribisha mkutano huo inajaa popote humo, ambapo maua mazuri yanalizunguka jumba hilo, na bendera za mataifa mbalimbali zinapepea. Kituo cha waandishi wa habari cha COP15 kikiwa kiini cha kutangaza habari za mkutano huo, kimefunguliwa kwa vyombo vya habari vya China na nchi nyingine mbalimbali, ili kuwatolea huduma waandishi wa habari wao. Vyombo vya habari 169, na waandishi wa habari 853 watakusanya habari papo hapo au kwa kupitia njia ya video kwenye mkutano huo.

Habari zinasema kuwa, mkutano huo wenye kaulimbiu ya “ustaarabu wa mazingira ya asili: Jenga pamoja jumuiya ya viumbe vya dunia”utafanya majumuisho kwa pande zote kuhusu uzoefu wa dunia nzima katika kulinda anuwai ya viumbe, na kupanga mfumo wa anuwai ya viumbe vya dunia baada ya mwaka 2020. Wajumbe wa nchi na sehemu karibu 200 zilizosaini mkataba watakwenda huko Kunming ili kujadilia mpango na mbinu za kulinda anuwai ya viumbe. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha