Reli ya kisasa iliyojengwa kwa msaada wa China yabadilisha maisha nchini Kenya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 30, 2021
Reli ya kisasa iliyojengwa kwa msaada wa China yabadilisha maisha nchini Kenya
Madereva wa China na Kenya wakijiandaa kuendesha treni katika kituo cha Nairobi cha reli ya SGR kati ya Mombasa na Nairobi mjini Nairobi, Mji Mkuu wa Kenya, Novemba 17, 2021. (Xinhua/Dong Jianghui)

NAIROBI - Concilia Owire alizaliwa na kukua katika kitongoji cha vijijini Magharibi mwa Kenya wakati ambapo wasichana wadogo walilazimika kupambana na kuzishinda imani hatari za kitamaduni, mfumo dume na vikwazo vya kifedha ili kutimiza ndoto zao za ajira.

Mtaalamu huyo wa uhandisi wa umeme akiwa na umri wa mwisho wa miaka ya 20 alipata hadhi ya mtu mashuhuri katika kijiji chake na kwingineko Mwaka 2017 alipojiunga na madereva wa kike wa treni wanaoongezeka katika Reli mpya ya SGR kati ya Mombasa na Nairobi iliyojengwa kwa msaada wa China.

“Naweza kusema nina furaha na bahati kuwa miongoni mwa kundi la kwanza la madereva wa kike wa treni nchini Kenya na nimeweza kujifunza mengi kutoka kwa kampuni na walimu wangu wa China,” alisema Owire.

Mwaka 2017, alishiriki katika mafunzo ya siku 50 nchini China ya kujifunza juu ya uendeshaji na ukarabati wa reli, na kujiandaa kwa ajili ya kuajiriwa katika huduma ya treni ya kisasa ambapo ustadi unathaminiwa sana.

Reli ya kisasa iliyojengwa kwa msaada wa China imefanya kazi kwa usalama zaidi ya miaka minne, hata ikiwa ni mshirika muhimu wa nchi hiyo katika kuleta mapinduzi ya usafiri, uunganishaji na biashara.

"Viashiria vya usafirishaji wa SGR na umuhimu wake kwa jamii umetambuliwa na wamiliki wa mizigo na abiria," inasema Kampuni ya Africa Star Railway Operation Company Limited (AfriStar) inayoendesha SGR.

Takwimu kutoka kwa waendeshaji wa SGR zinaonesha kuwa SGR ilikuwa imevunja rekodi kwa kusafirisha zaidi ya abiria milioni 6.4 kati ya Nairobi, Mji Mkuu wa Kenya, na mji wa pwani wa Mombasa tangu ilipozinduliwa Mwaka 2017 hadi Oktoba 31, 2021 ikilinganishwa na lengo la mwaka huu la kusafirisha abiria milioni 2.

Hivi sasa, kuna wastani wa treni sita za abiria na treni 17 za mizigo zinazofanya kazi kando ya ukanda wa Mombasa na Nairobi kila siku, ambazo zimepunguza muda wa safari huku zikihakikisha usalama wa wasafiri na mizigo.

Kampuni hiyo ya uendeshaji wa reli ya SGR imeeleza kuwa katika kipindi cha Mwaka 2021 pekee, hadi kufikia Oktoba 31, 2021, treni hiyo ya mizigo imesafirisha TEU 382,000, na kuongeza kuwa kuimarisha usalama wa mizigo, abiria na kulinda mazingira ya asili yaliyoko kando ya reli hiyo kumezingatiwa zaidi na kampuni hiyo.

Wakenya kutoka matabaka mbalimbali ambao wametumia huduma ya treni ya abiria kutoka Mombasa na Nairobi iliyozinduliwa Mwaka 2017 wamezungumza kwa furaha kuhusu namna reli hiyo ilivyo badilisha maisha yao katika nyanja mbalimbali.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha