Serikali za Mitaa katika Mkoa wa Guizhou nchini China zahimiza kupanda pilipili ya Sichuan ili kukuza uchumi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 17, 2022
Serikali za Mitaa katika Mkoa wa Guizhou nchini China zahimiza kupanda pilipili ya Sichuan ili kukuza uchumi
Mfanyakazi akiandaa pilipili ya Sichuan katika moja ya kampuni katika Mji Mdogo wa Zhennan, Wilaya ya Wuchuan, Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China, Juni 16, 2022. Ikiwa inaenea eneo kubwa la topografia ya karst na kupata athari zinazosababishwa na kuenea kwa jangwa lenye miamba, siku za nyuma Wilaya ya Wuchuan ilikuwa na mavuno kidogo ya kilimo. Serikali za mitaa zimehimiza kupanda pilipili ya Sichuan, zao la kibiashara linaloweza kustahimili sana kwenye maeneo ya jangwa lenye miamba, kama lengo la kukuza uchumi wa eneo hilo na kuhamasisha ustawi wa vijijini. Jumla ya eneo la shamba la pilipili ya Sichuan sasa linafikia hekta 15,000 katika wilaya hiyo. (Xinhua/Ou Dongqu)
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha