Mradi wa afya unaofadhiliwa na China wakamilika nchini Kenya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 01, 2022

(Picha kutoka Xinhua)

NAIROBI - Ubalozi wa China nchini Kenya na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) Alhamisi wiki hii wamefanya shughuli ya kusherehekea kukamilika kwa mafanikio mradi unaofadhiliwa na China wa kuhimiza afya ya uzazi, watoto wachanga na watoto nchini humo.

Mradi huo uliogharimu dola za kimarekani milioni 1 zilizotolewa na Serikali ya China, ulitekelezwa na UNICEF kati ya Januari 1, 2020 na Desemba 30, 2021, ukihusisha ununuzi na usambazaji wa vifaa tiba na dawa.

“Kukamilika kwa mafanikio kwa mradi huo ukiwa umefikia matokeo yaliyotarajiwa kunaonyesha ushirikiano mzuri kati ya China na UNICEF chini ya mfumo wa Ushirikiano wa Kusini na Kusini,” amesema Zhou Pingjian, Balozi wa China nchini Kenya, ambaye alishuhudia utiaji saini wa hati ya kuthibitisha kukamilika.

Kwa mujibu wa ofisi ya UNICEF nchini Kenya, mradi huo ulitoa vifaa tiba na mafunzo kwa vituo vya afya 159 katika kaunti 8 kote Kenya, na kuwanufaisha zaidi ya watu milioni 3.

“Kwa mchango na uungaji mkono wa China, UNICEF imekuwa ikiimarisha ujenzi wa vituo vya afya vya mashinani nchini Kenya na imepunguza ipasavyo idadi ya vifo vya wanawake wajawazito na watoto wakati wa janga la UVIKO-19,” amesema Maniza Zaman, mwakilishi wa UNICEF nchini Kenya.

(Picha kutoka Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha