Wapalestine wawili wafariki katika mapambano kati yao na askari wa Israeli Kaskazini mwa Kando ya Magharibi ya Mto Jordan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 25, 2022
Wapalestine wawili wafariki katika mapambano kati yao na askari wa Israeli Kaskazini mwa Kando ya Magharibi ya Mto Jordan
Wapalestine wakiangalia nyumba iliyoharibiwa na kikosi cha Israeli kwenye Nablus, Kando ya Magharibi ya Mto Jordan, Julai 24, 2022.

Madaktari na watu walioshuhudia walisema, mapema ya Jumapili ya wiki iliyopita, Wapalestine wawili walifariki katika mapambano makali kati yao na askari wa Israeli kwenye mji wa Nablus, Kaskazini mwa Kando Magharibi ya Mto Jordan.

Wizara ya Afya ya Palestine ilisema katika taarifa yake kuwa, askari wa Israeli waliwaua wanaume wawili wa Palestine wakati kikosi cha jeshi la Israeli kiliposhambulia mji huo, ambapo watu wengine 8 walijeruhiwa.

Wapalestina walioshuhudia hali ya huko walisema, kikosi cha jeshi la Israeli kilipoingia Nablus kwa ajili ya kutafuta Wapalestine waliosakwa na Israeli, watu wenye silaha wa Palestine na askari wa Israeli walipambama katika mji huo.

Jeshi la Israeli halijatoa maelezo mara moja kuhusu vifo vya Wapalesine hawa wawili. Lakini msemaji wa Jeshi alisema, kikosi cha jeshi la nchi hiyo kweli lilipambana na wapalestina wenye bunduki katika Nablus.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha