Waraka wa ulinzi wa Japani wa Mwaka 2022 unapuuza ukweli na kutoa maoni ya upande mmoja tu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 27, 2022

BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China, Wu Qian, Jumanne wiki hii alisema sehemu inayohusiana na China kwenye waraka wa ulinzi wa Japan wa Mwaka 2022 unaonyesha kutozingatia ukweli na umetoa maoni ya upande wake mmoja tu .

Wu alitoa kauli hiyo alipojibu maswali yaliyotolewa na waandishi wa habari kuhusu waraka huo.

Wu alisema Waraka huo umetoa kauli zisizo na uwajibikaji juu ya ulinzi wa nchi na maendeleo ya mambo ya kijeshi ya China, kufanya propaganda kuhusu kile kinachoitwa "tishio la kijeshi la China," kuchochea hali wasiwasi ya kikanda, na kuingilia kati mambo ya ndani ya China.

Aliongeza kuwa China inalaani vikali na inapinga kithabiti hoja hizo na imefikisha mawasilisho mazito kwa upande wa Japan.

Alisema, China inashikilia kufuata njia ya maendeleo ya amani, na inashikilia sera ya ulinzi wa nchi ya kujihami na kufuata mkakati wa kijeshi wa ulinzi wenye hamasa. Kama historia inavyoonyesha na itaendelea kutoa ushuhuda, majeshi ya China ni nguvu thabiti inayolinda amani ya Dunia.

“Kinyume chake, bila kujifunza somo kutoka kwenye historia, Japan inanyooshea kidole China na kufanya majaribio makali ya kukiuka utaratibu wa kimataifa wa baada ya Vita vya Pili vya Dunia, ambavyo vimefuatiliwa zaidi na jumuiya ya kimataifa na kuifanya ichukue tahadhari kubwa” Wu aliongeza.

Wu pia amekemea msimamo potovu wa Japan kuhusu mambo ya ndani ya China kama vile kuhusu Taiwan, Kisiwa cha Diaoyu na visiwa vinavyohusiana nacho, pamoja na visiwa vya Bahari ya Kusini na maeneo ya bahari yaliyoko karibu na bahari hiyo.

“Japan inapaswa kujikosoa kuhusu historia yake ya uvamizi , kuacha kucheza kadi ya mwathirika ili kupotosha jumuiya ya kimataifa na kuacha maneno na vitendo vyake visivyo sahihi kuhusu masuala yanayohusika ” aliasema Wu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha