China yataka Afrika iungwe mkono zaidi ili kuimarisha uwezo

(CRI Online) Agosti 09, 2022

Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun ambaye pia ni mwenyekiti wa zamu wa mwezi huu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuisaidia Afrika kuimarisha uwezo wa usalama na amani ya kudumu.

Akizungumza katika mjadala ulioitishwa na China wenye kaulimbiu “Amani na Usalama Afrika: Kujenga uwezo kwa ajili ya Amani ya kudumu”, Balozi Zhang amesema Baraza hilo linahitaji kufikiri kwa kina kuisaidia Afrika kutimiza amani ya kudumu.

Akitaja uzoefu wa maendeleo ya China, uzoefu wa ushirikiano kati ya China na Afrika, na mafunzo ya kihistoria kutoka sehemu mbalimbali duniani, Balozi Zhang amesema China inaamini kuwa kuisaidia Afrika kutimiza utulivu wa kudumu ni lazima kuongeza uwekezaji bila kusita, na kujenga msingi imara kwa ajili ya Afrika kuimarisha uwezo wake wa maendeleo na kuongeza nguvu yake ya kukabiliana na changamoto kutoka nje.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha