Mjumbe wa China aitaka kamati ya silaha za maangamizi kuzingatia mahitaji ya nchi zinazoendelea

(CRI Online) Desemba 02, 2022

Mjumbe wa China na naibu mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Geng Shuang, ameitaka kamati ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia silaha za maangamizi kuzingatia mahitaji ya nchi zinazoendelea.

Balozi Geng alitoa rai hiyo baada ya Baraza la usalama kupitisha kwa kauli moja azimio la kurejesha mamlaka ya Kamati ya 1540 kwa miaka 10. Kamati hiyo iliundwa mwaka 2004 kufuatilia utekelezaji wa Azimio namba 1540 la Baraza la Usalama, linalolenga kuzuia wahusika wasio wa serikali kupata silaha za nyuklia, kemikali au kibaolojia na njia za kuzitumia, na kuhimiza kuimarishwa kwa ushirikiano wa kimataifa katika suala hili.

Amesema kamati inapaswa kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu, kuongeza mchango wa msaada wa kiufundi na ushirikiano wa kimataifa, na kusaidia ipasavyo nchi zinazoendelea kuimarisha ujenzi wa uwezo wao wa kutekeleza hatua za kutoeneza silaha hizo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha