Reli ya mwendo wa kasi ya Guiyang-Nanning nchini China yaanza rasmi majaribio ya uendeshaji
 |
Mhudumu akifanya kazi kwenye treni ya majaribio katika Stesheni ya Guiyang Kaskazini huko Guiyang, Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China, Juni 26, 2023. Kuondoka kwa treni ya majaribio nambari 55311 kutoka Stesheni ya Guyang Kaskazini, kumeonesha kwamba reli ya mwendo kasi ya Guiyang-Nanning imeanza rasmi majaribio yake ya uendeshaji siku ya Jumatatu.
Reli hiyo iliyojengwa kutumika kwa treni zinazokimbia kwa kasi ya kilomita 350 kwa saa, inaunganisha Mji wa Guiyang wa Mkoa wa Guizhou na Mji wa Nanning wa Mkoa unaojiendesha wa Guangxi, nchini China. (Xinhua/Liu Xu) |
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)