Swala wa Tibet katika Mkoa wa Tibet nchini China waingia katika msimu wa kujamiiana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 19, 2023
Swala wa Tibet katika Mkoa wa Tibet nchini China waingia katika msimu wa kujamiiana
Kundi la swala jike wa Tibet wakikimbia kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mazingira asilia ya Qiangtang katika Mkoa unaojiendesha wa Tibet, Kaskazini-Magharibi mwa China, Desemba 16, 2023. Majira ya baridi ni msimu wa kujamiiana kwa swala wa Tibet wanaoishi katika Hifadhi ya Taifa ya Mazingira asilia ya Qiangtang, katika Mkoa unaojiendesha wa Tibet, Kaskazini-Magharibi mwa China. Msimu huo wa kujamiiana ambao ni wa wiki tatu ndiyo kipindi pekee katika mwaka mzima ambapo swala madume huonekana pamoja na majike. Ikijulikana kama "Pepo ya wanyama pori," Hifadhi hiyo ya Taifa ya Mazingira asilia ya Qiangtang ina aina zaidi ya 30 za wanyama pori walioorodheshwa kwenye orodha ya ulinzi wa kiwango cha kitaifa ya China, wakiwemo swala wa Tibet na ngo’ombe mwitu. (Jiang Fan/Xinhua)
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha