Watu wa Sudan Kusini waona matarajio makubwa katika kujifunza lugha ya Kichina

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 05, 2024

Kong Dejun (kushoto), mkurugenzi mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi wa Kimataifa katika Wizara ya Biashara ya China, akizungumza na mwanafunzi wa Sudan Kusini Mayiik Deng Mayiik katika Kituo cha Kujifunza Lugha ya Kichina kilichoko Shule ya Sekondari ya Juba, nchini Sudan Kusini, Machi 2, 2024. (Picha na Denis Elamu/Xinhua)

Kong Dejun (kushoto), mkurugenzi mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi wa Kimataifa katika Wizara ya Biashara ya China, akizungumza na mwanafunzi wa Sudan Kusini Mayiik Deng Mayiik katika Kituo cha Kujifunza Lugha ya Kichina kilichoko Shule ya Sekondari ya Juba, nchini Sudan Kusini, Machi 2, 2024. (Picha na Denis Elamu/Xinhua)

JUBA – Baadhi ya watu wa Sudan Kusini wanakimbilia kujiandikisha kwa masomo ya bila malipo ya lugha ya Kichina kwa kuwa fursa nyingi ambazo lugha hiyo inatoa katika nchi hiyo ambayo fursa za ajira ni chache kutokana na matatizo ya kiuchumi yaliyopo.

Amou Santo Domic, mwenye umri wa miaka 20, ni miongoni mwa wanafunzi wapya walioandikishwa tangu Januari katika Kituo cha Kujifunza Lugha ya Kichina kilichoko Shule ya Sekondari ya Juba chini ya Awamu ya Pili ya Mradi wa Elimu ya Ushirikiano wa Kiufundi unaosaidiwa na China nchini Sudan Kusini.

Amesema Jumamosi wakati wa ziara ya ujumbe wa ngazi ya juu kutoka Wizara ya Biashara ya China kukagua miradi inayosaidiwa na China nchini Sudan Kusini kwamba alijiandikisha katika kozi ya lugha ya Kichina ili kufahamu kidogo lugha hiyo kabla ya safari yake nchini China mwezi Julai kusoma shahada ya uhandisi wa petroli katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nanjing.

"Sababu iliyonifanya niwe hapa ni kwamba nitaenda China mwezi Julai kwa masomo yangu. Nilisikia kutoka kwa mtu wa Sudan Kusini ambaye alinitangulia kwenda China kwamba Wachina wanathamini lugha yao kuliko kitu chochote," Domic amesema huko Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini.

Amesema kujua Lugha ya Kichina kunatoa fursa zisizo na kikomo kwa sababu ya uwepo kampuni nyingi zinazomilikiwa na Wachina nchini Sudan Kusini na katika bara zima la Afrika.

Ujumbe wa China ukiongozwa na Kong Dejun, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Kimataifa katika Wizara ya Biashara ya China, uliwasili Juba Ijumaa ili kukagua maendeleo yaliyofikiwa katika miradi kadhaa inayofadhiliwa na China, ukiwemo Mradi wa Ushirikiano wa Kiufundi katika Elimu pamoja na Wizara ya Elimu ya Jumla na Mafunzo ya Sudan Kusini.

Awamu ya Pili ya mradi huo inahusisha kuandaa, kuhakiki, kuchapa, na kutoa vitabu vya kiada kwa baadhi ya shule za msingi na sekondari nchini Sudan Kusini na kuandaa programu za kuwajengea uwezo walimu na wasimamizi wa elimu na kazi nyinginezo.

Mayiik Deng Mayiik mwenye umri wa miaka 27, ambaye amekuwa miongoni mwa wanafunzi waanzilishi tangu kuzinduliwa kwa program hiyo ya kujifunza lugha ya Kichina na mawasiliano ya utamaduni mwezi Julai 2021, amesema kwamba kujifunza lugha ya Kichina kumemfanya apendwe na Wachina wengi ambao anapenda kuwatania kwa lugha fasaha ya Kichina.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Deng Jie)

Picha