Timu ya madaktari wa China yasaidia hospitali ya Ghana kuboresha huduma za radiolojia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 06, 2024

Du Yushan (Kulia), kiongozi wa kundi la 12 la timu ya madaktari wa China nchini Ghana, akiangalia mashine katika Hospitali ya LEKMA mjini Accra, Ghana, Machi 4, 2024. (Picha na Seth/Xinhua)

Du Yushan (Kulia), kiongozi wa kundi la 12 la timu ya madaktari wa China nchini Ghana, akiangalia mashine katika Hospitali ya LEKMA mjini Accra, Ghana, Machi 4, 2024. (Picha na Seth/Xinhua)

ACCRA - Kundi la 12 la timu ya madaktari wa China nchini Ghana limesaidia Hospitali ya LEKMA, hospitali kuu ambayo wanafanya kazi nchini humo kuboresha huduma zake za radiolojia katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, na kunufaisha maelfu ya wagonjwa wenyeji ambapo hospitali hiyo imekuwa ikikosa vifaa na teknolojia za radiolojia kwa miaka mingi, na kusababisha changamoto katika utambuzi wa magonjwa, amesema Du Yushan, kiongozi wa timu hiyo.

“Hospitali nzima ina mashine ya X-ray moja tu, lakini haimaanishi kwamba tungeshusha kiwango chetu. Badala yake tumefanikiwa kutumia mashine hiyo kupanua uchunguzi wa kimatibabu mfano upimaji wa umio,” Du ambaye pia ni mtaalamu wa radiolojia amesema katika mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua siku ya Jumatatu.

Du amesema timu ya madaktari wa China imeisaidia hospitali hiyo kuanzisha mfumo mzuri wa kuweka ripoti za radiolojia ili kuelezea vyema hali za wagonjwa, hivyo kutibu kwa usahihi zaidi magonjwa.

"Kwa magonjwa makali, sasa tunaweza kutoa matokeo ya uchunguzi mara moja, hali ambayo inasaidia madaktari kufanya matibabu ya haraka," Du ameongeza.

Dennis Amartey Ahia, naibu mkurugenzi mkuu wa radiografia katika hospitali hiyo, amesema hospitali hiyo imekuwa na bahati kwa miaka mingi kwamba kila kundi la timu ya madaktari wa China imekuwa na mtaalam wa radiolojia kati ya madaktari hao kutoa huduma hiyo muhimu kwa wagonjwa.

"Kwa ujumla, kuna wataalamu wachache sana wa radiolojia nchini, hivyo ushirikiano huu umekuwa msaada mkubwa kwetu katika kipindi cha miaka iliyopita," Ahia amesema.

Amesema msaada huo kutoka kwa timu ya madaktari wa China pia umeleta manufaa ya kiuchumi kwa wenyeji, ambao wanaweza kupata huduma katika hospitali hiyo kwa bei yenye ruzuku, na kuwasaidia kuokoa pesa.

Timu ya sasa ya madaktari wa China, ambayo inajumuisha wataalam 11 wa matibabu katika nyanja mbalimbali kutoka Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, itamaliza kazi yake ya mwaka mzima mwishoni mwa mwezi huu wa Machi.

Du Yushan (Kulia), kiongozi wa kundi la 12 la timu ya madaktari wa China nchini Ghana, akiangalia picha ya X-Ray katika Hospitali ya LEKMA mjini Accra, Ghana, Machi 4, 2024. (Picha na Seth/Xinhua)

Du Yushan (Kulia), kiongozi wa kundi la 12 la timu ya madaktari wa China nchini Ghana, akiangalia picha ya X-Ray katika Hospitali ya LEKMA mjini Accra, Ghana, Machi 4, 2024. (Picha na Seth/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Deng Jie)

Picha