Uchumi wa anga ya chini waongeza maendeleo ya sifa bora katika Mkoa wa Liaoning, China (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 13, 2025
Uchumi wa anga ya chini waongeza maendeleo ya sifa bora katika Mkoa wa Liaoning, China
Wafanyakazi wakifanya kazi ya kuunganisha sehemu za ndege kwenye kampuni ya Rhyxeon General Aircraft mjini Shenyang, Mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China, Mei 13, 2024. (Xinhua/Li Gang)

SHENYANG - Uchumi wa anga ya chini ukiwa nguvu mpya ya maendeleo ya uchumi na jamii, umechukuliwa na watu wengi kuwa shughuli mpya muhimu inayoibuka ya kimkakati.

Katika miaka ya hivi karibuni, Mkoa wa Liaoning kaskazini mashariki mwa China umekuwa ukitumia fursa kukuza ipasavyo uchumi wake wa anga ya chini. Mkoa huo umetumia vya kutosha hali inayofaa ya eneo lake la kijiografia na nguvu zake bora katika nyanja za usafiri wa anga na vyombo vya anga, umeweka mkazo wa maendeleo yake ya uchumi wa anga ya chini kwenye sekta za jumla za anga na droni, na kuboresha mazingira ya utumiaji kama vile uokoaji wa dharura, utalii wa kutazama mandhari, na ulinzi wa kilimo na misitu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha