Maendeleo ya uchumi wa anga ya chini katika sehemu mbalimbali za China (8)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 14, 2025
Maendeleo ya uchumi wa anga ya chini katika sehemu mbalimbali za China
Droni ya uchukuzi iliyopakiwa bidhaa na kuelekea Bandari ya Xuwen katika Mkoa wa Guangdong ikipaa kutoka nje ya ukumbi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Matumizi ya China (CICPE) mjini Haikou, Mkoani Hainan, kusini mwa China, Aprili 14, 2025. (Xinhua/Guo Cheng)

Ukiwa nguvu muhimu ya msukumo wa shughuli mpya ya kiuchumi, uchumi wa anga ya chini unachukuliwa na wengi kama viwanda muhimu vya kimkakati vinavyoibuka.

China imekuwa ikishuhudia maendeleo ya haraka ya teknolojia na viwanda katika uchumi wa anga ya chini katika miaka ya hivi karibuni, huku anga chini ya mita 1,000 kote nchini humo ikizidi kuwa "na pilika nyingi".

Kwa sasa, kampuni kubwa za upashanaji wa habari na mawasiliano za nchi hiyo, vilevile zile za betri yenye nguvu, magari na kampuni nyingine ziko zinashiriki kikamilifu katika uchumi huo wa anga ya chini, na mambo bunifu katika nyanja mbalimbali yanakusanyika katika viwanda vya uchumi wa anga ya chini.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha