Maendeleo ya uchumi wa anga ya chini katika sehemu mbalimbali za China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 14, 2025
Maendeleo ya uchumi wa anga ya chini katika sehemu mbalimbali za China
Droni iliyoundwa na Phoenix Wings, kampuni ya Vyombo vya Angani vya kubeba Mizigo Vinavyojiendesha bila Rubani (UAV) chini ya kampuni kubwa ya kusambaza vifurushi ya China ya SF Group, ikionekana katika picha kwenye hafla ya uzinduzi wa miradi kielelezo ya kundi la kwanza ya majaribio ya usimamizi wa uchumi wa anga ya chini (LAE) uliofanyika Hong Kong, kusini mwa China, Machi 20, 2025. (Xinhua/Chen Duo)

Ukiwa nguvu muhimu ya msukumo wa shughuli mpya ya kiuchumi, uchumi wa anga ya chini unachukuliwa na wengi kama viwanda muhimu vya kimkakati vinavyoibuka.

China imekuwa ikishuhudia maendeleo ya haraka ya teknolojia na viwanda katika uchumi wa anga ya chini katika miaka ya hivi karibuni, huku anga chini ya mita 1,000 kote nchini humo ikizidi kuwa "na pilika nyingi".

Kwa sasa, kampuni kubwa za upashanaji wa habari na mawasiliano za nchi hiyo, vilevile zile za betri yenye nguvu, magari na kampuni nyingine ziko zinashiriki kikamilifu katika uchumi huo wa anga ya chini, na mambo bunifu katika nyanja mbalimbali yanakusanyika katika viwanda vya uchumi wa anga ya chini.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha