

Lugha Nyingine
“Kijiji No. 1 cha Mashua ya Dragon cha China” chawa na pilika za uzalishaji mashua wakati Sikukuu ya Duanwu ikiwadia (4)
Kijiji cha Fangzhuang, kinachopatikana katika Wilaya ya Minhou ya Mji wa Fuzhou, Mkoani Fujian, ni kijiji kikubwa zaidi kwa uundaji wa mashua ya dragon nchini China, kikiwa na historia zaidi ya miaka 700 ya uundaji mashua za dragoni.
Wakati inapowadia Sikukuu ya Duanwu, sikukuu ya China ambapo watu hufanya mashindano ya mashua ya dragon kwa ajili ya kuisherehekea, mafundi kwenye karakana ya uundaji mashua za dragoni ya kijiji hicho wana pilikapilika za kufanya kazi ili kuharakisha kumaliza oda za mashua za sikukuu hiyo.
Kwa mujibu watakwimu, kijiji hicho kwa sasa hupokea oda kwa zaidi ya mashua 200 kila mwaka, ambayo yana thamani ya jumla ya karibu Yuan milioni 6 (sawa na Dola za Marekani 836,466).
Shughuli za kiutamaduni zafanyika kwenye Jukwaa la Russia na China mjini Khabarovsk, Russia
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma