Rais Xi Jinping asaini amri juu ya ulinzi wa miundombinu ya viwanda vya kijeshi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 27, 2025

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametia saini amri ya kutangaza kwa umma waraka wa sheria ya kulinda miundombinu muhimu ya viwanda vya kijeshi ya China. Baraza la Serikali la China na CMC kwa pamoja vimetangaza waraka huo.

Waraka huo utahusu majengo, maeneo, na miundombinu mingine inayotumika kwa utafiti, uzalishaji, majaribio na uhifadhi wa silaha na zana muhimu. Miundombinu hiyo pia inahusu majengo ya kumbukumbu za nyaraka na vituo vya data, vituo vya mawasiliano ya habari, vituo vya ufuatiliaji, na bandari maalum, magati, viwanja vya ndege, na njia za reli maalum.

Waraka huo umewekwa kanuni za hatua za usalama, zikiwemo za uanzishaji maeneo ya ulinzi kwa majengo na maeneo hayo, na bila idhini kutoka kwa mamlaka husika ya usimamizi, ni marufuku kwa watu binafsi, magari na meli kuingia maeneo hayo ya ulinzi. Pia umeweka kanuni za kutoruhusu kupiga picha, videografia, kurekodi sauti, kuchora, au kuweka kumbukumbu juu ya maeneo hayo yanayolindwa. Ukiukaji wa sheria husika unaweza kusababisha adhabu ya jinai.

"Mahitaji ya kulinda majengo na maeneo husika yanapaswa kutiliwa maanani wakati wa kuandaa mipango ya maendeleo ya uchumi na jamii” waraka huo unaeleza.

Wararka huo wa kisheria umewekwa vifungu 51 katika sura saba, na utafanya kazi kuanzia Septemba 15, 2025.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha