Rais Xi apongeza Chuo Kikuu cha Fudan kwa kuadhimisha miaka 120 tangu kuanzishwa kwake

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 27, 2025

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametuma barua ya pongezi kwa Chuo Kikuu cha Fudan jana Jumatatu, kuadhimisha miaka 120 tangu kuanzishwa kwake na kutoa pongezi kwa walimu, wanafunzi, wafanyakazi na wahitimu wa chuo kikuu hicho.

Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC)  katika barua hiyo amesema,“Katika miaka 120 iliyopita, Chuo Kikuu cha Fudan kimeenda sambamba na nyakati, kimeendeleza desturi fahari ya uzalendo na mienendo mizuri ya chuo kikuu, kimewaandaa vipaji vingi vya hali ya juu, kupata mafanikio mengi ya asili, na kufanya juhudi zake muhimu katika ujenzi wa nchi na maendeleo ya taifa la China.” 

Rais Xi ameelezea matumaini yake kwamba Chuo Kikuu cha Fudan, katika mwanzo wake mpya, kitaendelea kuwa thabiti katika kuwaandaa vipaji vingi kwa kutumia Fikra ya Ujamaa wenye Umaalum wa China kwa Zama Mpya.

"Chuo kikuu kinapaswa kuendeleza kwa kina mageuzi ya elimu na utafiti wa kisayansi, kuhimiza hali ya kusaidiana ya uvumbuzi wa kujitegemea wa kiteknolojia na kuwaandaa vipaji kwa kujitegemea, na kuchochea uvumbuzi katika falsafa na sayansi ya jamii," Rais Xi amesisitiza.

Pia amehimiza chuo kikuu hicho kuboresha siku hadi siku uwezo wake wa kutumikia mikakati mikuu ya kitaifa na maendeleo ya uchumi na jamii ya kikanda, na kutoa mchango mpya bila kusita kwa ajili ya kujenga nchi yenye nguvu na kustawisha Taifa la China kwa pande zote kwa kupitia ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.

Chuo Kikuu cha Fudan kilianzishwa mwaka 1905, ni chuo kikuu cha Mji wa Shanghai kinachojijengea kuwa na sifa bora ya juu, na kujitahidi kufanya uvumbuzi katika mambo mbalimbali.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha