

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China asema China na Malaysia kuingia kwa pamoja "Miaka 50 ya Dhahabu" kwa uhusiano wa pande mbili
![]() |
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim mjini Kuala Lumpur, Malaysia, Mei 26, 2025. (Xinhua/Li Xiang) |
KUALA LUMPUR - Waziri Mkuu wa China Li Qiang kwenye mkutano na Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim jana Jumatatu amesema kuwa China ingependa kushirikiana na Malaysia ili kuzidisha mawasiliano na ushirikiano katika sekta mbalimbali, na kwa pamoja kuingia "Miaka 50 ya Dhahabu" mipya kwa uhusiano wa pande mbili unaoongozwa kwa kanuni za kuheshimiana na kuaminiana, usawa na kunufaishana kwa pande zote.
Akikumbushia kuwa Rais Xi Jinping wa China alifanya ziara ya kiserikali nchini Malaysia mwezi uliopita, Li amesema kuwa pande zote mbili zilikubaliana kujenga jumuiya ya kimkakati ya ngazi ya juu ya China na Malaysia yenye mustakabali wa pamoja na kuweka ramani ya mwelekeo wa kimkakati wa maendeleo ya uhusiano wa pande mbili.
"China inapenda kushirikiana na Malaysia kutekeleza matokeo muhimu ya ziara hiyo ya kihistoria," amesema.
Amesema kuwa China inapenda kudumisha mawasiliano ya karibu ya ngazi ya juu na Malaysia, kuongeza mawasiliano ya kimkakati, na kuimarisha misingi wa kuaminiana kisiasa kwa jumuiya ya China na Malaysia yenye mustakabali wa pamoja.
Amehimiza pande hizo mbili kuendelea kupanua ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kwa kujikita katika maeneo mapya ya kisasa, ikiwa ni pamoja na uchumi wa kidijitali, uchumi wa kijani na akili bandia, kuhimiza maendeleo jumuishi ya minyororo ya viwanda na usambazaji na minyororo ya thamani, na kuendeleza kwa utulivu miradi mikubwa kama vile "Nchi Mbili, Bustani Pacha" na Reli Kiunganishi ya Pwani ya Mashariki, ili kuimarisha injini ya ukuaji uchumi wa jumuiya ya China na Malaysia yenye mustakabali wa pamoja.
"China inapenda kutekeleza vyema makubaliano ya kusameheana visa kati ya pande zote mbili na Malaysia, kuzidisha mawasiliano ya watu na ushirikiano katika utamaduni, elimu, afya, michezo na nyanja nyinginezo, na kuimarisha uhusiano kati ya watu na watu wa jumuiya ya China na Malaysia yenye mustakabali wa pamoja," Li amesema.
Amesema katika kukabiliana na kuongezeka kwa hali ya upande mmoja na kujilinda kibiashara na kudorora kuimarika kwa uchumi duniani, China, Jumuiya ya Mataifa ya Nchi za Asia Kusini-Mashariki (ASEAN) na nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba (GCC), washiriki wote na wanufaika wa utandawazi wa kiuchumi, wanapaswa kuimarisha uratibu na kwa pamoja kudumisha uwazi wa kikanda na mfumo wa kweli wa pande nyingi.
Kwa upande wake, Anwar amesema kuwa China ni jirani mwema na mshirika wa Malaysia.
“Ziara ya kihistoria ya Rais Xi nchini Malaysia mwezi uliopita ilikuwa na mafanikio makubwa,” amesema, akiongeza kuwa Malaysia inapenda kushirikiana na China ili kutekeleza kikamilifu matokeo ya ziara hiyo, kupanua zaidi ushirikiano katika biashara na uwekezaji, kuongeza miradi muhimu kama vile "Nchi Mbili, Bustani Pacha" na Reli Kiunganishi ya Pwani ya Mashariki, na kupanua ushirikiano katika maeneo kama vile nishati mpya, mambo ya fedha, rasilimali, akili bandia na maisha ya watu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma