

Lugha Nyingine
Afrika Kusini na Shirika la UN la Wanawake waandaa mkutano wa ushirikiano wa wadau wa G20 kuhusu ukuaji jumuishi
Wizara ya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu ya Afrika Kusini na Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake (UN Women) wameandaa mazungumzo ya wadau mjini Johannesburg jana Jumatatu ili kuhimiza ukuaji jumuishi chini ya Uenyekiti wa G20 wa nchi hiyo.
Kama sehemu ya vikao vya G20 vya Uwezeshaji wa Kikundi Kazi cha Wanawake, mkutano huo wa Ushirikiano wa Wadau wa G20 umepewa kauli mbiu ya "Kuendeleza Ukuaji Jumuishi kwa Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu kupitia Uenyekiti wa G20 wa Afrika Kusini 2025".
Waziri wa Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu wa Afrika Kusini Sindisiwe Chikunga, amesema jukwaa lao la G20 lazima lijikite katika uhalisia wa maisha ya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu, na si kama maelezo tu, bali kama msingi wa kuimarika na kukua kiuchumi.
Naye Naibu Waziri wa Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu wa nchi hiyo Mmapaseka Steve Letsike amesema jukumu la uongozi wa G20 la nchi hiyo pia linalenga kuleta mabadiliko ya kimfumo kwa ajili ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu duniani kote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma