Rais Xi na kiongozi wa Myanmar watumiana salamu za pongezi juu ya maashimisho ya miaka 75 tangu uhusiano wa kidiplomasia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 09, 2025

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China na kiongozi wa Myanmar Min Aung Hlaing wametumiana salamu za pongezi jana Jumapili juu ya maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, ambapo Rais Xi amesema kuwa, katika miaka hiyo 75 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, urafiki wa "Paukphaw" (kindugu) kati ya China na Myanmar umeshinda majaribu ya wakati na kuimarishwa zaidi. "Kwa kufuata Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani na Moyo wa Bandung zilizopendekezwa kwa pamoja, nchi hizo mbili zimeshikilia ujirani mwema na urafiki, kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana, na kuungana mkono kithabiti katika masuala yanayohusiana na maslahi yao ya kimsingi na mambo makubwa yanayofuatiliwa na pande zote, zikiweka mfano mzuri wa mawasiliano ya kirafiki kati ya nchi na nchi," amesema.

Rais Xi amekumbuka mkutano wake na Min Aung Hlaing nchini Russia mwezi Mei, wakati viongozi hao wawili walipofikia makubaliano muhimu juu ya kujenga jumuiya ya China na Myanmar yenye mustakabali wa pamoja.

Amesisitiza kuwa, China inaweka umuhimu mkubwa kwenye maendeleo ya uhusiano wake na Myanmar na inapenda kufanya juhudi pamoja na Myanmar kuchukuka maadhimisho hayo ya miaka 75 ya uhusiano wa kidiplomasia kuwa fursa ya kuhimiza kwa haraka ushirikiano wa kiwango cha juu katika ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kwa pamoja kutekeleza Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia na kusukuma upigaji hatua madhubuti katika kujenga jumuiya ya China na Mynmar yenye mustakabali wa pamoja, ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili.

Kwa upande wake, Min Aung Hlaing amesema kuwa ziara ya kihistoria ya Rais Xi nchini Myanmar mwaka 2020 ilifungua ukurasa mpya katika kujenga jumuiya ya Myanmar na China yenye mustakabali wa pamoja.

"Baada ya tetemeko kubwa la ardhi kutokea nchini Myanmar mapema mwaka huu, serikali na watu wa China walitoa msaada wa ubinadamu mara moja, ikionyesha vya kutosha urafiki wa kina kati ya watu wetu katika kupambana kwa pamoja na hali mbaya na kusaidiana wakati wa shida," amesema.

Min Aung Hlaing amepongeza mkutano wake na Rais Xi mjini Moscow wenye matunda, na kufikia makubaliano muhimu juu ya kuzidisha ushirikiano wa kimkakati.

Kiongozi huyo wa Myanmar amesema anatarajia kuharakisha ushirikiano na China katika sekta mbalimbali na kujenga uhusiano imara wa wenzi wenye nguvu kubwa na wa ushirikiano wa kunuifaishana zaidi.

Pia siku hiyo ya Jumapili, Waziri Mkuu wa China Li Qiang alitumiana salamu za pongezi na Min Aung Hlaing.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha