EAC yanadi chapa ya pamoja ya utalii wa kikanda kwenye maonyesho ya Karibu-Kilifair 2025

(CRI Online) Juni 09, 2025

Jumuiya ya Afrika Mashariki imetangaza kuwa inapanga kutangaza eneo hilo kama kivutio cha utalii cha pamoja.

Tangazo hilo limetolewa kwenye maonyesho makubwa zaidi ya utalii Afrika Mashariki, Karibu-Kilifair 2025, yaliyofungwa jana Jumapili mkoani Arusha, Tanzania.

Maonyesho hayo ya siku tatu yamevutia waonyeshaji zaidi ya 500 kutoka zaidi ya nchi 15, wakiwemo wanunuzi zaidi ya 1,000 wa kimataifa, wageni wa biashara, wanahabari na wakuu wa sekta ya utalii.

Mpango huo unalenga kuleta pamoja wadau wa utalii kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, zikiwemo bodi za utalii za kitaifa, waendeshaji watalii, wamiliki wa hoteli na watoa huduma, kwenye mfumo ulioratibiwa ili kuhimiza ushirikiano wa kuvuka mpaka, ujenzi wa chapa na vifurushi vya utalii kwa nchi mbalimbali.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha