Rwanda yajitoa ECCAS ikiishutumu DRC kuitumia jumuiya hiyo dhidi yake

(CRI Online) Juni 09, 2025

Rwanda imetangaza kuwa inajitoa kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika ya Kati (ECCAS) juzi Jumamosi, ikiishutumu nchi jirani yake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuitumia jumuiya hiyo dhidi yake kwa kuungwa mkono na baadhi ya nchi wanachama.

Tangazo hilo limekuja wakati mkutano wa 26 wa kilele wa jumuiya hiyo ulipokuwa ukifungwa mjini Malabo nchini Guinea ya Ikweta, ambao ulihudhuriwa na waziri mkuu wa Rwanda Edouard Ngirente.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Rwanda imesema, lengo la jumuiya hiyo limepotoshwa kidhahiri katika mkutano huo, wakati haki ya Rwanda ya kuchukua uenyekiti wa zamu imepuuzwa kwa makusudi ili kutekeleza amri ya DRC.

Mapema Jumapili Ikulu ya DRC ilitoa taarifa ikisema kutokana na hali ya sasa ya usalama Mashariki mwa nchi hiyo, viongozi wa ECCAS wamethibitisha kuwa DRC inakabiliwa na uvamizi kutoka Rwanda na wametoa wito kwa Rwanda kuondoa vikosi vyake kutoka kwenye ardhi ya DRC.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha