Ushirikiano wa Utamaduni na Utalii kati ya China na Kenya waonyeshwa kwenye tamasha la usiku

(CRI Online) Juni 09, 2025

Uhai wa ushirikiano kati ya China na Kenya kwenye utamaduni na utalii umeonyeshwa kikamilifu Ijumaa usiku kwenye Tamasha la Utamaduni na Utalii kati ya China na Kenya 2025 lililojumuisha maonyesho ya muziki, dansi na sarakasi.

Maofisa waandamizi wa serikali, wanadiplomasia, wasomi, viongozi wa tasnia na wananchi walihudhuria hafla ya ufunguzi wa Tamasha hilo, na kuadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa maonesho ya vikundi vya sarakasi kati ya China na Kenya.

Hafla hiyo iliandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Jinsia, Utamaduni, Sanaa na Urithi, Wizara ya Utalii na Wanyamapori ya Kenya, na Ubalozi wa China nchini Kenya.

Waziri wa Jinsia, Utamaduni, Sanaa na Urithi wa Kenya Hannah Wanjiku Cheptumo, amesifu ushirikiano unaostawi wa utamaduni na utalii kati ya China na Kenya, akiuelezea kuwa ni uhusiano wa kindugu wenye msingi wa kuaminiana na kunufaishana.

“Ushirikiano huu umeongeza maelewano na kukuza uhusiano kati ya watu” amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha