

Lugha Nyingine
Vyuo vikuu vya China vyafanya mashindano ya Kiswahili kuelekea maadhimisho ya siku Kiswahili duniani
(Picha/CRI)
Wanafunzi wachina wanaosoma somo la lugha ya Kiswahili, wameng'ara kwa kuonesha ustadi na weledi wao wa kuzungumza Kiswahili kwenye mashindano ya SHITU ya kuzungumza Kiswahili kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya China, 2025 yaliyofanyika Jumapili, Juni 8.
Akitoa hotuba yake kwenye mashindano hayo yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing (BFSU) kwa ushirikiano na Baraza la Kiswahili la Taifa, Tanzania (BAKITA), kuelekea Siku ya Kiswahili Duniani, Balozi wa Tanzania nchini China, Khamis Mussa Omar amewapongeza washiriki kwenye mashindano hayo kwa maandalizi mazuri na kuongea Kiswahili kwa ufasaha mkubwa.
Naye Profesa Zhao Gang, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing akitoa neno la ukaribisho alisema mashindano hayo yanawezesha vijana wachina kuboresha ujuzi wao wa lugha na kuimarisha uelewa wao wa ustaraabu wa Afrika kupitia mawasiliano.
Katika mashindano hayo, nafasi ya kwanza kwa wanafunzi wa madarasa ya juu imechukuliwa na Meng Wenhui (Nyota) kutoka Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Xi’an. Na kwa upande wa madarasa ya chini, imekwenda kwa Li Yuanhang (Nina) wa Chuo Kikuu Cha Lugha za Kigeni cha Beijing.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma