

Lugha Nyingine
Mkutano wa kwanza wa utaratibu wa mashauriano kuhusu uchumi na biashara kati ya China na Marekani wafunguliwa London
Wajumbe wa China na Marekani wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mkutano wa kwanza wa utaratibu wa mashauriano kuhusu uchumi na biashara kati ya China na Marekani mjini London, Uingereza, Juni 9, 2025. (Xinhua/Li Ying)
LONDON - Mkutano wa kwanza wa utaratibu wa mashauriano kuhusu uchumi na biashara kati ya China na Marekani umefunguliwa jijini London, Uingereza jana Jumatatu, ambapo Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), anafanya mazungumzo na upande husika wa Marekani.
Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akipeana mkono na Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent kabla ya mkutano wa kwanza wa utaratibu wa mashauriano kuhusu uchumi na biashara kati ya China na Marekani mjini London, Uingereza, Juni 9, 2025. (Xinhua/Li Ying)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma