Jimbo la California, Marekani lamshtaki Trump kwa amri "kinyume na kisheria" ya Walinzi wa Taifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 10, 2025

Askari wa Kikosi cha Ulinzi wa Taifa cha California wakikabiliana na waandamanaji mbele ya Kituo cha Kizuizi cha Serikali Kuu cha Los Angeles, mjini Los Angeles, California, Marekani, Juni 8, 2025. (Picha na Qiu Chen/Xinhua)

SACRAMENTO, Marekani - Jimbo la California la Marekani limeushtaki mahakamani utawala wa Rais Donald Trump jana Jumatatu kwa kutuma askari wa Kikosi cha Ulinzi wa Taifa cha jimbo hilo mjini Los Angeles kutokana na kuwepo kwa maandamano dhidi ya msako wa ukamataji wa wahamiaji unaofanywa na serikali kuu, likiiita kitendo hicho "hatua isiyo na shaka kuelekea udikteta.”

Gavana Gavin Newsom na Mwanasheria Mkuu Rob Bonta wa Jimbo la California wametangaza Jumatatu kuwa wamefungua kesi dhidi ya utawala wa Trump kukomesha "uchukuaji haramu na usio wa lazima" wa Walinzi wa Taifa wa jimbo hilo, ambao wamesema "umeongeza machafuko na ghasia katika eneo la Los Angeles."

Kesi hiyo, ambayo inawataja Rais Donald Trump, Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth, na Wizara ya Ulinzi, inadai kuwa uchukuaji huo unakiuka Katiba ya Marekani na unavuka mamlaka ya Rais ya Kifungu cha 10, si tu kwa sababu uchukuaji huo umefanyika bila ya ridhaa au maoni ya gavana, kama sheria ya serikali kuu inavyotaka, lakini pia kwa sababu haikuwa halali, kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka ofisi ya gavana huyo ya jana Jumatatu.

Maandamano hayo awali yalianza katika kukabiliana na operesheni za usimamizi wa utekelezaji sheria ya uhamiaji. Katika siku za hivi karibuni, maafisa wa utawala huo wamekuwa wakielekeza juhudi zao katika miji mikubwa inayoongozwa na Chama cha Democrat, ukiwemo Los Angeles, Chicago na New York.

Mvutano kati ya waandamanaji hao na wasimamizi wa utekelezaji sheria uliongezeka siku ya Ijumaa wiki iliyopita, huku baadhi ya waandamanaji wakirusha vitu na polisi kujibu kwa mipira ya pilipili na vifaa vya mlipuko wa kutoa mwanga.

Katika kukabiliana na hali hiyo, Rais Trump aliamuru kutumwa kwa walinzi wa taifa 2,000 Jumamosi. Maandamano hayo yaliongezeka zaidi siku ya Jumapili, huku kukiwa na kuongezeka kwa watu wengi na makabiliano makali kati ya waandamanaji na maafisa hao wa usimamizi wa utekelezaji sheria.

Askari wa Kikosi cha Ulinzi wa Taifa cha California na maafisa wa polisi wakiwa katika ulinzi kwenye Kituo cha Kizuizi cha Serikali Kuu cha Los Angeles, mjini Los Angeles, California, Marekani, Juni 8, 2025. (Picha na Qiu Chen/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha