

Lugha Nyingine
Wajumbe watafuta suluhu zinazojikita kwa wakulima katika Jukwaa la Teknolojia ya Kilimo la Afrika nchini Rwanda
Wajumbe wanaohudhuria Jukwaa la Teknolojia ya Kilimo la Afrika (ACAT) wametoa wito wa uwekezaji wa dharura katika teknolojia za kilimo zinazotilia maanani wakulima ili kuwezesha wakulima wadogo barani Afrika.
Katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika Jumatatu mjini Kigali, washiriki wamesisitiza umuhimu wa kuwapa wakulima maarifa na nyenzo sahihi za kutatua changamoto tatanishi katika kilimo cha kisasa.
Akihutubia mkutano huo, Waziri wa Kilimo na Raslimali za Wanyama wa Rwanda, Mark Cyubahiro Bagabe, amesema uwezeshaji wa wakulima unatimizwa kupitia kuwapa ujuzi na rasilimali ili kuwasaidia kutoa maamuzi sahihi ya kuboresha mazoea yao ya kilimo na kutatua changamoto zinazowakabili katika kilimo cha kisasa.
Jukwaa la ACAT ni moja ya majukwaa makubwa ya Afrika kwa ajili ya kuhimiza teknolojia za kisasa za kilimo na sera za kiutendaji zinazowezesha sekta ya kilimo kuwa jumuishi, yenye ufanisi na himilivu zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma