Benki ya Dunia yasema Watanzania milioni 1.9 kunufaika na mpango wake mpya wa ufadhili

(CRI Online) Juni 10, 2025

Benki ya Dunia imetoa taarifa ikisema Watanzania takriban milioni 1.9 wanatarajiwa kunufaika na uwezo na utayari ulioimarishwa wa kukabiliana na maafa chini ya mpango mpya wa ufadhili wa shirika hilo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa jana Jumatatu, ufadhili huo wa mkopo wa dola za kimarekani milioni 300 unajumuisha dola milioni 100 za Ufadhili wa Sera za Maendeleo kama uungaji mkono wa bajeti, na dola nyingine milioni 200 zilizotengwa kwa ajili ya Chaguo la Kukopa Kuepusha Majanga kutoka Shirika la Maendeleo ya Kimataifa (IDA).

Shirika hilo limeeleza kuwa lengo la ufadhili huo ni kuimarisha uhimilivu wa kiuchumi na kuongeza uwezo wa Tanzania wa kiufundi, kifedha na kitaasisi wa kukabiliana na hatari zinazohusiana na tabianchi, mambo ya fedha na maafa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha