

Lugha Nyingine
Naibu Waziri Mkuu wa China akutana na wageni wa nchi za nje wanaohudhuria mkutano wa BRI
CHENGDU – Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amefanya mikutano kwa nyakati tofauti jana Jumanne na wageni kadhaa wa nchi za nje ambao wako nchini China kuhudhuria Mkutano wa pili wa Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) kuhusu mawasiliano ya Sayansi na Teknolojia mjini Chengdu, Mkoani Sichuan.
Akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Serbia Marina Ragus, Ding amesema kuwa China inapenda kushirikiana na Serbia kutekeleza maafikiano muhimu yaliyofikiwa kati ya wakuu wa nchi hizo mbili, kuunga mkono masuala yanayofuatiliwa na maslahi ya msingi ya kila upande wao, kuzidisha ushirikiano wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kugeuza ushirikiano wa uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia kuwa eneo jipya la ukuaji wa uhusiano wa pande mbili, na kuhimiza mafanikio zaidi katika ujenzi wa jumuiya ya China na Serbia yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.
Kwa upande wake Ragus amesema kuwa Serbia inathamini sana urafiki wake na China, inafuata bila kuyumba kanuni ya kuwepo kwa China moja, na inapenda kuimarisha ushirikiano wa kivitendo na China katika nyanja kama vile uwekezaji, uchumi na biashara, na sayansi na teknolojia, kwa lengo la kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya nchi hizo mbili.
Wakati akikutana na Naibu Waziri Mkuu wa Uzbekistan Ramatov Achilbay Jumaniyazovich, Ding amesema China inapenda kushirikiana na Uzbekistan ili kuongeza hali ya kuaminiana kwao kisiasa na urafiki wa muda mrefu, kuzidisha kuwiana kwao kwa mikakati ya maendeleo, na kuhimiza ushirikiano wa kina, mkubwa katika nyanja kama vile muunganisho wa miundo mbinu, uchumi na biashara na uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia chini ya mfumokazi wa ushirikiano wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.
Naye Ramatov amesema, Uzbekistan inapenda kuzidisha ushirikiano wa kivitendo na China chini ya mwongozo wa makubaliano ya kimkakati yaliyofikiwa kati ya wakuu wa nchi hizo mbili, na kuhimiza maendeleo ya ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili.
Katika mazungumzo na Makamu Rais wa Iran anayeshughulikia mambo ya Sayansi, Teknolojia na Uchumi Hossein Afshin, Ding amesema, kwa kuongozwa na maafikiano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, China inapenda kufanya juhudi za pamoja na Iran ili kutekeleza vema mpango wa ushirikiano wa kina kati ya China na Iran, kuhimiza ushirikiano wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kutumia ipasavyo zaidi uwezo wa ushirikiano katika nyanja ya sayansi na teknolojia ili kuleta manufaa zaidi halisi kwa watu wa nchi hizo mbili.
Afshin amesema, Iran inaweka umuhimu mkubwa kwenye maendeleo ya uhusiano wa pande mbili na China na inapenda kuimarisha uhusiano kati ya watu na nchi hiyo, kuhimiza utekelezaji wa mpango wa ushirikiano wa kina, na kupata maendeleo mpya katika ushirikiano wa sayansi na teknolojia.
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
LEGOLAND Shanghai Resort kuanza shughuli za majaribio kabla ya kufunguliwa Julai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma