Shughuli ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mazungumzo kati ya Ustaarabu zafanyika UN (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 11, 2025
Shughuli ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mazungumzo kati ya Ustaarabu zafanyika UN
Wasanii wakifanya maonyesho ya sanaa ya kupigana kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Juni 9, 2025. (Xinhua/Li Rui)

UMOJA WA MATAIFA – Shughuli mbalimbali zimefanyika Jumatatu kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York ili kuadhimisha mwaka wa kwanza ya Siku ya Kimataifa ya Mazungumzo kati ya Ustaarabu ambapo ni pamoja na mazungumzo yenye kauli mbiu ya "Kuhimiza mazungumzo kati ya ustaarabu, kuimarisha mshikamano na ushirikiano wa kimataifa," ambayo yaliandaliwa na ujumbe wa kudumu wa China,  Misri, Peru, Hispania na Uzbekistan kwenye Umoja wa Mataifa, pamoja na Muungano wa Ustaarabu wa Umoja wa Mataifa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi alitoa ujumbe kwa njia ya video kwenye mazungumzo hayo ya kaulimbiu ambapo katika ujumbe wake amesema kuwa mazungumzo kati ya ustaarabu mbalimbali ni dhamana ya amani, kichocheo cha maendeleo na daraja la urafiki, akisema ni wakati muafaka wa kuendeleza mazungumzo kati ya ustaarabu mbalimbali.

Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ametoa wito wa kufanya juhudi za kudumisha usawa na kuhimiza mawasiliano ya kati ya tamaduni mbalimbali.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema katika ujumbe wake kwamba mazungumzo ni muhimu kwa ajili ya kujenga madaraja ya maelewano na kuaminiana, akisema kuwa "Siku hii ya Kimataifa ni wito kwa kuchukua hatua -- kusikiliza, kuzungumza, kuwasiliana."

Akitoa wito wa kudhamiria tena kwa maadili na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Philemon Yang amesema, "Tusherehekee umoja na uanuwahi wa ustaarabu, na kuhimiza uvumilivu, mazungumzo na ujumuishaji kuelekea dunia bora kwa wote."

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na mwakilishi mkuu wa Muungano wa Ustaarabu wa Umoja Mataifa Miguel Angel Moratinos, pamoja na wanadiplomasia waandamizi kutoka Misri, Peru, Hispania na Uzbekistan, pia wamesisitiza umuhimu wa mazungumzo kati ya ustaarabu mbalimbali.

Shughuli nyingine, onyesho la sanaa lenye kaulimbiu ya "Zaidi ya mipaka: Kufuma tamaduni kupitia kujieleza kisanii," likiwa ni pamoja na maonyesho ya muziki, dansi na sanaa ya kupigana kujihami, imeonyesha matarajio ya pamoja ya binadamu kwa maendeleo yenye mapatano.

Likiwa lililopendekezwa na China na kuungwa mkono na nchi zaidi ya 80, azimio lililopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka jana liliiteua Juni 10 kila mwaka kuwa Siku ya Kimataifa ya Mazungumzo kati ya Ustaarabu Mbalimbali. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha