

Lugha Nyingine
Reli ya kisasa ya Kenya iliyojengwa kwa msaada wa China yaadhimisha miaka 8 ya uendeshaji bila kukoma (4)
NAIROBI - Sherehe ya kuadhimisha miaka minane ya uendeshaji bila kukoma wa Reli ya Kisasa ya SGR ya Mombasa-Nairobi iliyojengwa kwa msaada wa China imefanyika jijini Nairobi Jumanne, ambapo wakati akihutubia hafla ya sherehe hiyo, Balozi wa China nchini Kenya Guo Haiyan ameipongeza reli hiyo ya SGR kwa kuwa mradi kinara wa Pendekezo lililotolewa na China la Ukanda Mmoja, Njia Moja, na pia ni hatua muhimu katika safari ya Kenya kuelekea mageuzi ya kiuchumi.
“China inapenda kufanya juhudi pamoja na Kenya katika kutekeleza makubaliano muhimu ya wakuu wa nchi hizo mbili na kuimarisha ushirikiano katika ujenzi wa miundombinu,” amesema Guo.
"Sasa miaka minane imepita na bado tunaendelea kuwa na nguvu kubwa, na tumepata maendeleo dhahiri ya kukidhi matarajio ya wateja waliokuwa nayo ya miaka mingi iliyopita," amesema Abdi Bare, mwenyekiti wa Shirika la Reli la Kenya.
Bare ameongeza kuwa huduma zote za usaifiri wa abiria na usafirishaji wa mizigo za reli hiyo ya SGR zimeleta mabadiliko makubwa katika usafiri na usafirishaji nchinikwetu, zikihimiza mafungamano ya mawasiliano, biashara na maendeleo ya viwanda.
Hadi kufikia mwisho wa Mei 2025, reli hiyo ya SGR ilikuwa imesafirisha abiria zaidi ya milioni 15.3 na mizigo yenye uzito wa tani zaidi ya milioni 40.3.
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
LEGOLAND Shanghai Resort kuanza shughuli za majaribio kabla ya kufunguliwa Julai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma