Fundi mwenye umri wa miaka 68 achangia uhai wa ufundi wa kuunda mashua ya Shaoxing, China (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 13, 2025
Fundi mwenye umri wa miaka 68 achangia uhai wa ufundi wa kuunda mashua ya Shaoxing, China
Qian Shoutang akiunda mashua yenye paa nyeusi pamoja na wanafunzi wake mjini Shaoxing, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China, Juni 12, 2025. (Xinhua/Weng Xinyang)

Mashua yenye paa nyeusi ni chombo cha usafiri cha kipekee chenye historia ndefu mjini Shaoxing, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China. Ufundi wa kuunda mashua hiyo uliorodheshwa kwenye orodha ya mali ya urithi wa utamaduni usioshikika ya mkoa wa huo wa Zhejiang mwaka 2009.

Qian Shoutang mwenye umri wa miaka 68, ni mrithi mwakilishi wa ufundi huo mjini Shaoxing. Qian alizaliwa katika familia yenye ufundi wa jadi wa kuunda mashua hiyo ya paa nyeusi, amekuwa akijishughulisha na kuunda mashua kwa zaidi ya miaka 50. Kwa sasa, Qian na wanafunzi wake kila mwaka wanaunda mashua hizo za paa nyeusi zaidi ya kumi, hasa kwa ajili ya matumizi katika maeneo ya mandhari ya kuvutia.

"Kwa kuwa watu wengi zaidi, hasa kizazi cha vijana, wanavutiwa na utamaduni wa jadi, ni jambo lenye umuhimu kwangu kurithisha ufundi huo na kuwafundisha vijana," Qian amesema. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha