Rais wa Nigeria azindua barabara kuu iliyojengwa na kampuni ya China katika mji mkuu, Abuja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 13, 2025
Rais wa Nigeria azindua barabara kuu iliyojengwa na kampuni ya China katika mji mkuu, Abuja
Picha hii iliyopigwa tarehe 4 Juni 2025 ikionyesha barabara kuu ya N16 mjini Abuja, Nigeria. (Kampuni ya CGC Tawi la Nigeria/kupitia Xinhua)

ABUJA - Rais Bola Tinubu wa Nigeria Jumatano alizindua barabara kuu ya N16 yenye urefu wa kilomita 3.64, iliyojengwa na Kampuni ya China ya CGC Tawi la Nigeria na kupongeza kukamilika kwa barabara kuu hiyo ya Abuja, akisema kwamba ujenzi wa miundombinu ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Uzinduzi huo umeorodheshwa kama moja ya miradi muhimu ya Mamlaka ya Utawala wa Eneo la Mji Mkuu, kuadhimisha mwaka wa pili tangu rais huyo aingie madarakani.

Barabara hiyo ya N16 inaunganisha sehemu kadhaa za Abuja, na barabara za juu za makutano na barabara ndogo za kuingiza magari kwenye barabara kuu katika Wilaya ya Maitama, moja ya maeneo yenye wakazi na pilika nyingi sana mjini humo.

"Ambacho awali kilikuwa kiunganishi kilichokosekana sasa ni muundombinu wa kisasa, wenye kazi nyingi, na wa kudumu, ateri imepatikana kikamilifu," Rais Tinubu amesema, akiongeza kuwa mradi huo wa ujenzi umethibitisha dhamira ya utawala wake kwa mageuzi chini ya Ajenda ya Matumaini Mapya.

"Barabara hii itapunguza msongamano wa magari kuzunguka Katikati ya Abuja na kuboresha muunganisho kwenye wilaya zinazoendelea kama vile Katampe, Jahi, na Bwari. Itachochea ukuaji wa makazi na biashara huku ikitumika kama msingi wa ujumuishaji wa baadaye wa mji," rais huyo amesema.

Rais Tinubu amepongeza uhamishaji wa jamii za wenyeji na fidia kwa wakazi walioathiriwa na ujenzi huo, akihimiza wananchi kulinda na kutumia barabara hiyo kwa uangalifu ili kuleta ukuaji wa uchumi, ujumuishaji wa kijamii, na fursa za kiuchumi.

Baraza Tendaji la Serikali Kuu ya Nigeria lilitoa kandarasi hiyo kwa CGC Tawi la Nigeria Septemba 2024, na ujenzi ulianza mwezi mmoja baadaye. Mradi huo umekamilika ndani ya muda wa miezi minane, miezi minne kabla ya kipindi cha mwaka mmoja cha kufanya kazi.

Zhong Xiang, mkurugenzi mkuu wa CGC Tawi la Nigeria, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba moyo wa kuaminiana na urafiki kati ya China na Nigeria umeimarisha imani yao.

"Katika kipindi chote cha ujenzi, tulitengeneza fursa za ajira zaidi ya 1,300 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, ikihimiza kwa kiasi kikubwa shughuli za kiuchumi za wenyeji," amesema. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha