

Lugha Nyingine
Mwanafunzi wa Nigeria atafuta utimizaji wa ndoto za udaktari nchini China (2)
Ekpene Mabel Solomon, mwenye umri wa miaka 21, alizaliwa nchini Nigeria na sasa ni mwanafunzi anayechukua kozi ya matibabu katika Chuo Kikuu cha Matibabu cha Changsha, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China.
Kabla ya kuja China, Ekpene alikuwa amejifunza kuhusu utamaduni wa jadi wa Wachina kupitia televisheni na intaneti na akapendezwa nao sana. Mwaka 2022, alifaulu mtihani wa uteuzi na akashinda udhamini wa masomo kusoma katika chuo kikuu hicho.
Baada ya kuingia chuoni, amekuwa akisoma masomo mbalimbali yakiwemo ya historia ya Tiba ya Jadi ya China (TCM) na Baduanjin ambayo ni michezo ya jadi ya mazoezi ya Aerobiki ya China inayojulikana kwa manufaa yake kwa afya. Akiwa na alama za juu, Ekpene alitunukiwa ufadhili wa masomo wa mkoa wa Hunan wa 2023-2024 kwa wanafunzi wa kimataifa.
Wakati wa masomo yake nchini China, yeye anafurahia kutembelea makumbusho na kusafiri ili kuelewa zaidi utamaduni wa China. Katika wakati wake wa masomo , binti huyo mpenda mitindo pia huandaa video za urembo na mtindo wa maisha kwenye mitandao ya kijamii.
Ingawa imebaki miaka mitatu zaidi hadi kuhitimu, Ekpene tayari amepanga mipango yake ya siku za baadaye. Anatarajia kuendelea na masomo nchini China, na baadaye kurejea nchini mwake kuchangia huduma ya afya.
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
LEGOLAND Shanghai Resort kuanza shughuli za majaribio kabla ya kufunguliwa Julai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma