

Lugha Nyingine
Uchumi wa China wadumisha hali tulivu mwezi Mei huku kukiwa na hali ya nje isiyokuwa na uhakika
![]() |
Picha iliyopigwa Juni 16, 2025 ikionyesha mandhari ya gati la kontena la Bandari ya Tangshan mjini Tangshan, Mkoani Hebei kaskazini mwa China. (Picha na Liu Mancang/Xinhua) |
BEIJING - Uchumi wa China umeendelea kupanuka kwa hatua madhubuti mwezi Mei, kutokana na hatua zinazoendelea za kisera ambazo zimesaidia kudumisha kufufuka huku kukiwa na hali ya kukosekana uhakika duniani, takwimu rasmi zilizotolewa jana Jumatatu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) zimeonyesha kuwa viashiria muhimu vya kiuchumi -- uzalishaji viwandani, mauzo ya rejareja, uwekezaji na huduma -- viliongezeka mwezi uliopita, wakati huohuo soko la ajira likiendelea na mwelekeo wa utulivu.
Msemaji wa NBS Fu Linghui amesema kuwa ingawa mazingira ya kimataifa yanabadilika badilika, uchumi wa China umeonyesha unyumbufu na uhai mkubwa, kutokana na juhudi za serikali za kupanua mahitaji ya ndani na kudumisha utulivu wa ajira, biashara, masoko na matarajio.
Matumizi ya wanunuzi ya China mwezi Mei yalirekodi ukuaji wake mkubwa zaidi katika takriban miezi 18 iliyopita, huku mauzo ya rejareja ya bidhaa za watumiaji yakipanuka kwa asilimia 6.4 mwezi Mei kuliko mwaka jana wakati kama huo, na kuongezeka asilimia 1.3 kuliko Aprili.
Sekta ya huduma iliongezeka kwa kasi, huku faharisi ya uzalishaji wa huduma ikipanda kwa asilimia 6.2 mwezi uliopita, ikiongezeka kutoka ukuaji wa asilimia 6 uliorekodiwa mwezi Aprili. "Kuongezeka matumizi ya nyumbani na kusafiri kwa likizo vimesababisha ukuaji wa haraka wa huduma," Fu amebainisha.
Uzalishaji viwandani ulipanda kwa asilimia 5.8 mwaka hadi mwaka mwezi Mei, takwimu hizo za NBS zinaonyesha, huku utengenezaji vifaa na teknolojia ya hali ya juu ukiongoza kwa asilimia 9 na asilimia 8.6 ya ukuaji mtawalia na uwekezaji wa mali zisizohamishika katika miezi mitano ya kwanza ya 2025 ukiongezeka kwa asilimia 3.7 kuliko kipindi kama hicho mwaka jana.
Kwa upande wa soko la ajira, takwimu hizo zinaonesha kuwa wastani wa kiwango cha ukosefu wa ajira mijini nchini China ulifikia asilimia 5 mwezi Mei, ukipungua kwa asilimia 0.1 kuliko Aprili.
Fu amewaambia waandishi wa habari kuwa ufanisi huo thabiti wa uchumi wa Mei umetokana na juhudi endelevu za sera kuu, ambayo ziliwezesha upanuzi wa mahitaji, kukua kwa uzalishaji na matarajio yaliyoboreshwa, na kuibua uhai wa kiuchumi.
Akitazama siku za usoni, Fu amesema kuwa hali ya kimsingi ya maendeleo ya uchumi wa muda mrefu wa China haijabadilika, akirejelea kasi ya maendeleo imara ya nchi hiyo, sera madhubuti za kuunga mkono ukuaji uchumi na kuimarishwa kwa uvumbuzi, ambavyo vyote vinatoa uungaji mkono kwa ukuaji wa uchumi wenye sifa bora.
"Katika nusu ya kwanza ya 2025, uchumi wa China unatarajiwa kudumisha uthabiti wake wa ujumla huku ukipata maendeleo tulivu," amesema.
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
LEGOLAND Shanghai Resort kuanza shughuli za majaribio kabla ya kufunguliwa Julai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma