

Lugha Nyingine
Namna mnyororo wa kiviwanda kati ya China na Afrika unavyohimiza ukuaji wa bara (4)
NAIROBI – Thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilifikia dola za Kimarekani bilioni 295.56 mwaka 2024, ikiongezeka kwa asilimia 4.8 kuliko mwaka uliopita wakati kama huo, ikimaanisha mwaka wa 16 mfululizo kwa China kubakia kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika.
Hivi sasa, kutokana na mipango kazi 10 ya ushirikiano, kampuni za China na Afrika zinaimarisha ushirikiano katika mnyororo mzima wa kiviwanda, ikihimiza maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili na kutoa msukumo mpya kwa ukuaji endelevu wa uchumi.
Kuongeza uzalishaji ndani barani Afrika
Nchini Cote d'Ivoire, Eneo Maalum la Viwanda la PK24 nje kidogo ya Abidjan, mji mkuu wa kiuchumi wa nchi hiyo, kuna pilika nyingi. Kiwanda kipya cha kusindika kakao, kiwanda cha kwanza cha kisasa cha nchi hiyo kinachomilikiwa na serikali, kinakaribia kuzinduliwa.
Kikiwa kimejengwa na Kampuni ya viwanda vyepesi ya China ya uhandisi wa ubunifu ya Nanning, kituo hicho kinaweza kusindika tani 50,000 za kakao kwa mwaka na kuhifadhi tani 140,000. Hii inaonyesha hatua kubwa katika harakati za nchi hiyo kuendeleza mnyororo wa thamani wa kimataifa.
"Hatimaye tunasindika kakao katika ardhi yetu," amesema Ettien Kouakou Camille, mkulima mwenyeji huku akijivuna.
Mageuzi kama haya yanafanyika katika bara zima. Katika Mkoa wa Mashariki mwa Rwanda, shamba la Gashora PLC linapanua uzalishaji wa pilipili kali kwa uungaji mkono kutoka kampuni ya China ya Maendeleo ya Kimataifa ya Kilimo cha Kisasa ya Hunan. Ushirikiano kati ya kampuni hizo ni pamoja na kuboresha miundombinu, kama vile uhifadhi wa baridi, vifaa vya kukausha na mashamba yaliyopanuliwa.
"Soko la China ni kubwa. Tuliona mahitaji makubwa ya pilipili kavu ya Rwanda," amesema Dieudonne Twahirwa, mkurugenzi mkuu wa shamba hilo.
Kuwaandaa watu wenye ujuzi
Licha ya miundombinu, ushirikiano kati ya China na Afrika umetilia mkazo mafunzo ya ufundi stadi na kuwaandaa watu wenye ujuzi.
Katika kitongoji cha kusini cha mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo, wafanyakazi wenyeji zaidi ya 3,000 katika kiwanda cha nguo cha cashmere kinachomilikiwa na Kundi la Kampuni za King Deer Cashmere la Mkoa wa Mongolia ya Ndani wa China wanageuza nyuzi za hali ya juu za kufumia kuwa bidhaa zilizotayari kuuzwa nje.
Kampuni za China pia zinaendesha mahitaji ya ujuzi wa ufundi kote Afrika. Mipango ya kinara kama Karakana za Luban yanahimiza mafunzo ya vitendo, yanayozingatia viwanda katika nchi kadhaa za Afrika.
Kuunganisha masoko ya kimataifa
Ushirikiano kati ya China na Afrika pia unawezesha bidhaa za Afrika kusafirishwa kwenye masoko ya kimataifa kupitia majukwaa mbalimbali.
Nchini Kenya, jukwaa la biashara ya mtandaoni la Kilimall lililoanzishwa na kampuni ya China limekuwa moja ya wauzaji ongozi wa reja reja mtandaoni katika Afrika Mashariki. Mmoja wa wafanyabiashara wake wakuu, Hoswell Macharia, anauza TV zinazozalishwa nchini humo na kampuni iliyowekezwa kwa mtaji kutoka China ya Vitron, thamani yake ya mauzo ya mwaka imefikia shilingi milioni 96 za Kenya (dola za Kimarekani kama 745,000).
Makamu Mkuu wa Kilimall Wu Mixiang amesema kuongezeka kwa uwepo wa wazalishaji wa China barani Afrika kunamaanisha wauzaji wenyeji wanapata bidhaa bora na za bei nafuu, ambayo inageuka kuwa faida halisi kwa watumiaji.
Kampuni nyingine kubwa za mtandaoni za China kama Shein na Temu pia zinapanuka barani Afrika, zikiunganisha kampuni za Afrika na uchumi wa kidijitali duniani.
Kuanzia miundombinu na mafunzo hadi uzalishaji na mauzo ya kimataifa, ushirikiano wa kiviwanda kati ya China na Afrika unazidi kuimarika. Wakati bara hilo likibadilika kutoka kwenye mauzo ya malighafi hadi kunufaika na uzalishaji thamani, ushirikiano huu unasaidia kuweka msingi kwa ajili ya ukuaji wa muda mrefu, wa kujitegemea na mustakabali mzuri.
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
LEGOLAND Shanghai Resort kuanza shughuli za majaribio kabla ya kufunguliwa Julai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma