Maisha ya kuhamahama ya mfugaji katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 18, 2025
Maisha ya kuhamahama ya mfugaji katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
Picha iliyopigwa tarehe 14 Juni, 2025 ikionyesha wafugaji wakisubiri kuingia kwenye hifadhi ya taifa ya mazingira ya asili ya Gogodtai Han Ul, Mkoa wa Mongolia ya Ndani, kaskazini mwa China. (Xinhua/Ma Jinrui)

Saintsogt, mwenye umri wa miaka 55, mfugaji katika eneo la Bayin-undur la Ar Horqin Banner, Mkoa wa Mongolia ya Ndani Kaskazini mwa China, yuko katika pilika nyingi za uhamaji wa kila mwaka wa majira ya joto unaochukua umbali wa kilomita takriban 100. Kwa miongo minne iliyopita, amekuwa akikamilisha uhamaji huo kila mwaka.

Malisho ya mifugo ya Saintsogt ni sehemu ya Mfumo wa Kuhamahama wa Mbuga ya Ar Horqin, ambao uliorodheshwa kuwa mojawapo ya maeneo ya Mifumo Muhimu ya Urithi wa Kilimo Duniani (GIAHS) na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Mei 20, 2022. Wafugaji katika eneo hilo bado wanahifadhi mila ya jadi ya kuhamahama hadi leo.

"Muda wa safari umefupishwa hadi siku tatu kutoka nane. Mvua hufanya malisho kukua vizuri, na mifugo ina malisho ya kutosha" amesema Saintsogt.

Mwaka huu, wafugaji kutoka kaya zaidi ya 1,200 na mifugo 128,000 katika eneo hilo la Bayin-undur wamehama. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha