Wilaya ya Caoxian ya China yajenga mnyororo kamili wa viwanda vya vazi la kijadi la Hanfu (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 23, 2025
Wilaya ya Caoxian ya China yajenga mnyororo kamili wa viwanda vya vazi la kijadi la Hanfu

Wilaya ya Caoxian katika Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China imekuwa ikitumia nguvu ya msingi wake wa biashara ya mtandaoni kujijenga kuwa kituo cha kimataifa cha Hanfu, ambayo ni mavazi ya kijadi ya China. Wilaya hiyo imejenga muundo kamili wa mnyororo wa viwanda vinavyofanya usanifu wa mavazi, utengenezaji, ulinzi wa hakimiliki, na uuzaji kidijitali.

Mavazi hayo ya Hanfu yanayotengenezwa katika wilaya hiyo, haswa "sketi ya uso wa farasi" (katika lugha ya Kichina Mamianqun), yamevutia macho ya watu kwa kupitia kuonekana kwenye mashindano ya usanifu wa mavazi ya Kichina na Wiki ya Mitindo ya Milan, Italia. Nguo hizo zimekuwa zikisafirishwa kuuzwa nje hadi Australia, Canada, na Umoja wa Ulaya, zikizalisha mapato yenye thamani ya Yuan bilioni 12 (dola za Kimarekani takriban bilioni 1.6) katika mauzo ya jumla mwaka 2024.

Ikichochewa na uamsho wa kiutamaduni unaohimizwa na vijana, viwanda vinavyostawi vya Hanfu vya Wilaya ya Caoxian ni mfano wa mafanikio ya mafungamano ya urithi wa jadi na uvumbuzi wa kidijitali. Si tu imebadilisha urembo wa kale kuwa alama za utambulisho wa kisasa wa Wachina kwenye jukwaa la kimataifa bali pia imekuwa injini mpya ya kuongeza mapato ya watu wa wilaya hiyo na kuendeleza ustawi wa vijijini. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha